Mkutano wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa wafunguliwa Kenya kwa wito wa kulinda afya ya sayari ya Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 09, 2025

Picha hii iliyopigwa Desemba 8, 2025 ikionyesha hafla ya kufunguliwa kwa mkutano wa saba wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA-7) jijini Nairobi, Kenya. (Xinhua/Yang Guang)

Picha hii iliyopigwa Desemba 8, 2025 ikionyesha hafla ya kufunguliwa kwa mkutano wa saba wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA-7) jijini Nairobi, Kenya. (Xinhua/Yang Guang)

NAIROBI – Mkutano wa saba wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA-7) umefunguliwa rasmi jana Jumatatu jijini Nairobi, Kenya, ambao umetoa wito wa kupata ufumbuzi wa kudumu kwa matishio yanayozidi kuwa mbaya dhidi ya sayari ya Dunia.

Wajumbe karibu 6,000, wakiwemo maofisa wa mazingira, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, sekta za taaluma, viwanda, na watu wa jamii kutoka nchi zaidi ya 170, wanahudhuria mkutano huo wa siku tano unaofanyika chini ya kaulimbiu ya "Kusukuma Mbele Utatuzi Endelevu kwa Kujenga Sayari Himilivu ya Dunia ."

Katika hotuba yake ya video, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed amesisitiza dharura ya kukabiliana na matishio ya ikolojia kama vile mabadiliko ya tabianchi, upotevu wa mazingira ya kuishi, na uchafuzi wa mazingira ili kuhakikisha kupata mustakabali himilivu kwa binadamu.

"Lazima tuchukue hatua kwa hali ya dharura ili kulinda afya ya sayari yetu ya Dunia. Sasa ni wakati wa kuwekeza katika tabianchi tulivu na mifumo ya ikolojia inayostawi, na kuhakikisha ushirikiano wa pande nyingi unatoa matokeo halisi kwa watu na sayari ya Dunia," amesema Mohammed.

Kikiwa ni chombo cha juu zaidi cha kufanya maamuzi duniani juu ya masuala yanayohusu mazingira, mkutano huo wa UNEA umekuwa ukifanyika tangu mwaka 2014 ukiwa na ujumbe wa jumla wa nchi zote wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa.

Wakati wa mkutano huo wa mwaka huu, wajumbe watajadili miswada ya maazimio 15 na miswada ya maamuzi matatu yanayotoa wito wa kuimarisha ulinzi wa mito ya barafu, kutimiza uzalishaji endelevu wa migodi na madini, na kupunguza athari ya kiikolojia ya AI.

Usimamizi endelevu wa rasilimali za maji baridi zinazovuka mipaka, kubadilisha muundo wa uchumi kwa kuelekea wa mzunguko, kuhifadhi spishi ya ndege wanaohamahama, usimamizi wa bahari, na haki ya tabianchi pia ni mada muhimu katika majadiliano.

Mwenyekiti wa UNEA-7 Abdullah Bin Ali Al-Amri amesema jukwaa hilo litatoa msukumo kwenye ajenda ya kijani duniani, chini ya uelekezaji wa njia ya kisayansi na moyo wa maoni moja.

“Kuimarisha makubaliano ya mazingira ya pande nyingi, kuhimiza ujumuishaji na ushirikiano, kutakuwa mada muhimu zaidi kwenye mkutano ili kusaidia kupanga njia himilivu kwa sayari ya Dunia na wakazi wake” Abdullah amesema.

Deborah Barasa, katibu wa baraza la mawaziri katika Wizara ya Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi, na Misitu ya Kenya, amesema kwamba UNEA-7 itajengwa kwenye msingi wa juhudi zinazoendelea duniani ili kuanzisha mustakabali wa sayari ya Dunia baadaye ulio mzuri zaidi, salama zaidi, kijani zaidi, na himilivu zaidi.

Picha hii iliyopigwa Desemba 8, 2025 ikionyesha mandhari ya nje ya ukumbi wa mkutano wa saba wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA-7) jijini Nairobi, Kenya. (Xinhua/Yang Guang)

Picha hii iliyopigwa Desemba 8, 2025 ikionyesha mandhari ya nje ya ukumbi wa mkutano wa saba wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA-7) jijini Nairobi, Kenya. (Xinhua/Yang Guang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha