Tanzania yatangaza maandamano ya leo Desemba 9 kuwa ni kinyume na sheria

(CRI Online) Desemba 09, 2025

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Tanzania, George Simbachawene, amehimiza wananchi kuepuka maandamano yaliyopangwa kufanyika leo Jumanne Desemba 9, akiyatangaza kuwa ni kinyume cha sheria na kuonya kuwa ushiriki wake utachukuliwa kuwa ni kosa la uhalifu.

Akizungumza na wanahabari mjini Dar es Salaam jana Jumatatu, Simbachawene amesema waandaaji wa maandamanao hayo wameshindwa kupata vibali vinavyohitajika ama kuweka wazi malengo, wafadhili, au njia ya maandamano hayo.

Tangazo hilo limekuja wiki chache baada ya vurugu kubwa zilizotokea katika sehemu mbalimbali za Tanzania Oktoba 29, zikisababisha vifo, uharibifu wa mali na usumbufu mkubwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha