Lugha Nyingine
Rais wa sasa wa Cote d’Ivoire aapishwa kwa muhula mpya wa miaka mitano
(CRI Online) Desemba 09, 2025
Rais wa sasa wa Cote d'Ivoire, Alassane Ouattara, ameapishwa mbele ya Baraza la Katiba la nchi hiyo mjini Abidjan jana Jumatatu, kwa muhula wa nne wa miaka mitano, baada ya kushinda uchaguzi kwa asilimia 89.77 ya kura.
Akihutubia baada ya kuapishwa mjini Abidjan, Rais Ouattara ameeleza mafaniko yaliyopatikana katika miaka 15 ya utawala wake, ikiwemo urejeshaji wa mamlaka ya nchi, amani, na ukuaji wa kasi wa uchumi.
Amesema katika miaka mitano ijayo, Cote d'Ivoire itaanza safari ya mageuzi yanayoongozwa na uchumi, ufanisi zaidi katika viwanda na ushindani zaidi kutoka sekta binafsi, na miundombinu ya kisasa ya nishati, uchukuzi na ya kidijitali.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



