Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China afanya mazungumzo na viongozi wa mashirika makubwa 10 ya kiuchumi duniani
Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang jana Jumanne mjini Beijing amefanya mazungumo ya “1+10” na viongozi wa mashirika makubwa 10 ya kiuchumi duniani, ikiwemo Benki Mpya ya Maendeleo, Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa, Shirika la Biashara Duniani, Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia, na Shirika la Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo.
Kwenye mazungumzo hayo Waziri Mkuu Li amesema, China siku zote itaendelea kufungua mlango wake kwa upana zaidi kwa dunia, na inakaribisha kampuni nyingi zaidi za nje kuwekeza katika soko la China.
Viongozi wa mashirika hayo wamesema, wana nia ya kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na China katika maeneo mbalimbali, kushirikiana na China kudumisha ushirikiano wa pande nyingi na mfumo wa biashara huria ili kuhimiza ukuaji wa uchumi duniani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



