Vitu vya msaada wa dharura wa kibinadamu vya China kwa ajili ya mafuriko vyawasili Colombo, Sri Lanka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 10, 2025

Picha hii iliyopigwa Desemba 8, 2025 ikionyesha hafla ya makabidhiano ya vitu vya msaada wa dharura wa kibinadamu kwa ajili ya mafuriko vilivyotolewa na serikali ya China mjini Colombo, Sri Lanka. (Xinhua/Xu Han)

Picha hii iliyopigwa Desemba 8, 2025 ikionyesha hafla ya makabidhiano ya vitu vya msaada wa dharura wa kibinadamu kwa ajili ya mafuriko vilivyotolewa na serikali ya China mjini Colombo, Sri Lanka. (Xinhua/Xu Han)

COLOMBO - Vitu vya msaada wa dharura wa kibinadamu kwa ajili ya mafuriko vilivyotolewa na serikali ya China vimewasili Colombo Jumatatu asubuhi na kukabidhiwa kwa upande wa Sri Lanka ambapo Balozi wa China nchini Sri Lanka Qi Zhenhong, Waziri wa Bandari na Usafiri wa Anga wa Sri Lanka Anura Karunathilake, na Naibu Waziri wa Ulinzi Aruna Jayasekera walihudhuria hafla ya makabidhiano.

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano, Karunathilake ametoa shukrani za dhati kwa msaada huo wa wakati na wa ukarimu wa China, akisema kuwa vitu hivyo vilivyowasilishwa Jumatatu ndivyo hasa Sri Lanka inahitaji sana.

Amesisitiza kwamba China siku zote imetoa msaada kwa Sri Lanka katika kila inapokumbwa na magumu kwa miaka mingi. Amesema, katika kukabiliana na janga la sasa, serikali ya China, kampuni za China na watu wa China nchini Sri Lanka wametoa msaada mkubwa.

Ameishukuru serikali ya China na watu wake kwa msaada wao wa kujitolea na akasisitiza matumaini yake kwamba urafiki kati ya Sri Lanka na China utaendelea.

Kwa upande wake Balozi Qi amesema kwamba, katika kukabiliana na janga hilo kubwa la asili, idara zote husika za China zilichukua hatua haraka kutoa msaada kwa marafiki wa Sri Lanka. Amesema vitu hivyo, ambavyo vinajumuisha mahema, mashuka, majaketi ya kuokoa maisha, na mablanketi, ni sehemu ya msaada wa kibinadamu wa serikali ya China kwa Sri Lanka.

“Kampuni za China na Wachina wanaoishi nchini Sri Lanka pia wamechukua hatua za kivitendo kufanya juhudi za uokoaji kwa waathirika wa janga nchini,” amesema, akisisitiza kwamba msaada huo wa pande zote wa China kwa mara nyingine unaonyesha kwamba China ni rafiki mzuri anayeaminika na wa kutegemeka wa rafiki wa kweli wa Sri Lanka.

“China, kama ilivyo wakati wote, itaendelea kuisaidia Sri Lanka iwezekanavyo, kufanya kazi pamoja ili kushinda mambo magumu, na kujenga kwa pamoja jumuiya ya China na Sri Lanka yenye mustakabali wa pamoja,” ameongeza.

Kwa mujibu wa Kituo cha Usimamizi wa Maafa cha Sri Lanka, nchi hiyo hivi karibuni ilipata uharibifu mkubwa kutokana na hali mbaya ya hewa iliyosababishwa na Kimbunga Ditwah, ambacho kimesababisha vifo vya watu zaidi ya 600, kuathiri watu zaidi ya milioni 2, kubomoa nyumba zaidi ya 4,000 na kuharibu kwa sehemu za nyumba zaidi ya 60,000 kote nchini.

Picha hii iliyopigwa Desemba 8, 2025 ikionyesha vitu vya msaada wa dharura wa kibinadamu kwa ajili ya mafuriko vilivyotolewa na serikali ya China mjini Colombo, Sri Lanka. (Xinhua/Xu Han)

Picha hii iliyopigwa Desemba 8, 2025 ikionyesha vitu vya msaada wa dharura wa kibinadamu kwa ajili ya mafuriko vilivyotolewa na serikali ya China mjini Colombo, Sri Lanka. (Xinhua/Xu Han)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha