Lugha Nyingine
Jukwaa la Afrika kuhusu wanawake, amani na usalama lafunguliwa nchini Tunisia
Jukwaa la Sita la Ngazi ya Juu la Afrika kuhusu Wanawake, Amani na Usalama limefunguliwa nchini Tunisia jana jumanne, likisisitiza hitaji la uratibu wa pande nyingi ili kukabiliana na changamoto za pamoja.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia, mkutano huo wa siku mbili unatoa jukwaa muhimu la kusukuma mbele ajenda juu ya haki, amani na usalama wa wanawake.
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia Mohamed Ali Nafti amesisitiza kuwa, hali ya sasa ya dunia inahitaji mshikamano na hatua zilizoratibiwa zaidi ili kukabiliana na changamoto za pamoja, hususan amani na usalama.
Pia amesisitiza kuwa, amani ya kudumu inahitaji mbinu za kina na za kuzuia, ambazo zinashughulika na vyanzo vya kimfumo kama vile hali ya ukosefu wa usawa na umasikini, ambavyo vinachochea kutengwa na kutojumuishwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



