Kampuni ya Ujenzi ya China kujenga makao makuu ya forodha ya Cameroon

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 10, 2025

Wawakilishi kutoka serikali ya Cameroon na Kampuni ya Uhandisi wa Mashine ya China (CMEC) wakiweka jiwe la msingi la ujenzi wa makao makuu ya Kurugenzi Kuu ya Forodha ya Cameroon mjini Yaounde, mji mkuu wa Cameroon, Desemba 9, 2025. (Xinhua/Kepseu)

YAOUNDE - Serikali ya Cameroon imeweka jiwe la msingi jana Jumanne kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu ya Kurugenzi Kuu ya Forodha ya Cameroon ambapo Waziri wa Fedha wa nchi hiyo Louis Paul Motaze amesema kwenye hafla hiyo kwamba kandarasi ya ujenzi wa mradi huo imepewa Kampuni ya Uhandisi wa Mashine ya China (CMEC).

"Serikali (ya Cameroon) inazingatia sana uhusiano kati ya China na Cameroon. Mradi huu wa ujenzi wa makao makuu ya Kurugenzi Kuu ya Forodha ya Cameroon ni kielezo kamili na mafanikio ya ushirikiano wa pande mbili," Motaze amesema.

Ameongeza kuwa, jengo hilo jipya linatarajiwa kupamba mji mkuu wa Yaounde, ikiwa ni sehemu ya mpango mpana wa kuboresha huduma za serikali.

Cui Haozhen, mwakilishi kutoka CMEC, amesema kampuni hiyo imeazimia kujenga eneo hilo kuwa alama mpya ya mji mkuu, ikitoa mchango wa China katika kuboresha utawala wa Cameroon.

"Tutahamasisha timu zetu bora, teknolojia na nyenzo za kuaminika zaidi, na usimamizi wa hali ya juu kutoka China ili kuhakikisha kikamilifu ubora, usalama, na kuharakisha upigaji hatua wa mradi," Cui amesema katika hotuba yake kwenye hafla hiyo.

"Tutashirikiana kwa karibu na mteja, timu ya usimamizi, wahandisi, na washirika wote kwa uwazi na ufanisi ili kuhakikisha kwamba mradi huu unakuwa mfano wa mradi-salama, wa kuaminika, na wa sifa bora," ameongeza.

Mradi huo, ulioko Yaounde karibu na Ikulu ya Rais, utatoa mazingira ya kisasa ya ofisi na kuongeza ufanisi wa kiutawala.

Waziri wa Fedha wa Cameroon Louis Paul Motaze akitoa hotuba kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya makao makuu ya Kurugenzi Kuu ya Forodha ya Cameroon mjini Yaounde, mji mkuu wa Cameroon, Desemba 9, 2025. (Xinhua/Kepseu)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha