Lugha Nyingine
China yaipinga vikali Uingereza kwa kufanya uchochezi wa kisiasa kwa kutumia suala la usalama wa mtandao
(CRI Online) Desemba 11, 2025
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Guo Jiakun jana amesema, China inapinga vikali hatua ya Uingereza ya kufanya uchochezi wa kisiasa kwa kutumia suala la usalama wa mtandao.
Habari zinasema, jumanne wiki hii serikali ya Uingereza ilitangaza kuweka vikwazo dhidi ya makampuni mawili ya China, na kudai kuwa makampuni hayo yalifanya mashambulizi ya mtandao dhidi ya Uingereza na washirika wake, na kitendo hicho kinahusiana na serikali ya China.
Akijibu tuhuma hizo, Bw. Guo Jiakun amesema China inapinga na kupambana kithabiti na shughuli za udukuzi kwa mujibu wa sheria, na wakati huo huo inapinga kabisa uenezaji wa taarifa za uongo kwa sababu za kisiasa.
Bw. Guo pia amesema, China ni mwathirika mkubwa wa mashambulizi ya mtandao.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



