Msemaji: Japan ni mchochezi wa tukio la “Mwanga wa rada”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 11, 2025

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya China jana Jumatano alisema kuwa, katika suala kuhusu ati "mwanga wa rada", ni upande wa Japan ambao ulisumbua kwa makusudi na kueneza habari potovu, upande huo ndio mchochezi wa ulaghai wa kisiasa, na lazima ubebe lawama zote.

Msemaji huyu Guo Jiakun alisema hayo kwenye mkutano wa kawaida na waandishi wa habari, ambapo alisema, vyombo vya habari vya China vimeshatoa video na rekodi za sauti kuhusu tukio la "mwanga wa rada" na kila kitu husika, na ukweli wa mambo umeonekana waziwazi.

Alisema, China imefanya mazoezi na mafunzo kwenye maeneo husika ya anga na bahari kwa kufuata kabisa sheria na kanuzi za kimataifa, akiongeza kuwa, mazoezi ya China yanafuata kanuni za utaalamu, yakiwa ni ya salama na ya kujizuia, hakuna mengine zaidi ya hayo.

"Jana, upande wa Japan ulisema haukufahamishwa na China kuhusu mazoezi ya urukaji wa ndege hapo kabla. Lakini leo ulikiri kuwa walikuwa wamepata habari husika kabla ya mazoezi hayo ya China. Na upande wa Japan unakataa kueleza sababu zake za kupeleka ndege za kivita kuingia kwenye eneo la mazoezi ya China wakati wakiwa wamepokea habari husika, na kufanya vitendo vya upelelezi wa kiadui na wa kusumbua tena na tena, ili kusababisha hali ya msukosuko na kuvutia ufuatiliaji wa vyombo vya habari. Je, upande wa Japan unakusudia kuchepusha yanayofuatiliwa zaidi na kujaribu kupotosha ukweli wa mambo mbele ya jumuiya ya kimataifa?

Guo alisema, upande wa China unataka jumuiya ya kimataifa kujua hali halisi na iliyopotoshwa, na kutodanganywa na upande wa Japan, akisisitiza washirika wa Japan wakae macho zaidi na wasipotoshwe na Japan.

Msemaji huyu alisema, upande wa Japan unapaswa kuelewa kwa usahihi sababu kweli za hali ya taabu ya hivi sasa katika uhusiano kati ya China na Japan, kujikosoa kwa kina, kurekebisha makosa yake, na kurudisha maeneo ya makosa aliyosema Waziri Mkuu Sanae Takaichi kuhusu Taiwan.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha