Lugha Nyingine
UNICEF yatafuta dola za kimarekani bilioni 7.66 kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa watoto katika mwaka 2026
(CRI Online) Desemba 11, 2025
Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limezindua ombi la Mpango wa Kibinadamu kwa Watoto katika mwaka 2026 jana jumatano, likitafuta dola za kimarekani bilioni 7.66 ili kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa watoto katika nchi na maeneo 133 mwaka ujao.
Akizungumza na wanahabari katika mkutano wa kila siku, Naibu Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema, wakati ufadhili wa dunia umepungua na huduma za msingi kuzorota, mahitaji ya kibinadamu kwa watoto yanaendelea kuongezeka.
Amesema UNICEF inazitaka serikali na wafadhili kuongeza ufadhili wa pande nyingi kwa mwaka, kuunga mkono wenzi wa ndani, kudumisha kanuni za kibinadamu na kuhakikisha mahitaji ya watoto yanapatikana.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



