Lugha Nyingine
Thailand yasema Migogoro ya mpakani na Cambodia yamesababisha watu zaidi ya 400,000 wa Thailand kukimbia makazi yao

Picha hii iliyochukua kutoka video inaonyesha msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Thailand, Surasant Kongsiri, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Bangkok, Thailand, Desemba 10, 2025. (Picha na Xinhua)
BANGKOK – Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Thailand, Surasant Kongsiri, alisema jana Jumatano kwamba hali ya mapigano inayoendelea kwenye mpaka na Cambodia yamewalazimu wakazi zaidi ya 400,000 wa Thailand katika mikoa saba kuhamishwa.
Kamandi ya Eneo la 2 la Jeshi la Thailand ilisema kwenye mitandao ya kijamii kwamba, saa 2:40 hivi asubuhi kwa saa za huko, roketi za BM-21 zilizorushwa kutoka upande wa Cambodia ziliangukia karibu na hospitali moja ya Mkoa wa Surin, na kusababisha wagonjwa na wafanyakazi wa hospitali hiyo kuhamishiwa kwenye maeneo salama.
Vyombo vya habari vya Thailand vinasema kuwa, mapigano mapya ya mpakani kati ya Thailand na Cambodia yamesababisha shule zaidi ya 800 na hospitali nyingi kufungwa kwa muda katika mikoa yanayopo mpakani mwa Thailand.
Mgogoro wa mpakani kati ya Cambodia na Thailand uliibuka upya tangu Jumapili alasiri. Nchi hizo mbili zilishutumu nchi nyingine kuanzisha mapigano haya.

Picha hii ikionyesha wagonjwa na wafanyakazi wa hospitali wakihamishwa kwenda maeneo salama ambapo roketi za Cambodia ziliangukia karibu, katika Mkoa wa Surin, Thailand, Desemba 10, 2025. (Jeshi la Thailand / Kupitia Xinhua)

Picha hii ikionyesha hali ndani ya hospitali ambapo roketi za Cambodia ziliangukia karibu, katika Mkoa wa Surin, Thailand, Desemba 10, 2025. (Jeshi la Thailand / Kupitia Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



