Marufuku ya kwanza duniani ya Australia kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii kwa walio chini ya umri wa miaka 16 yaanza kutekelezwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 11, 2025

SYDNEY – Marufuku ya Australia kwa watoto wenye umri chini ya miaka 16 kutumia mitandao ya kijamii imeanza kutekelezwa Jumatano. Majukwaa 10 makubwa ikiwa ni pamoja na Facebook, YouTube, TikTok, X yanatakiwa kuwazuia watoto wenye umri chini ya miaka 16 kuwa na akaunti.

Katika ujumbe wa video kwa wanafunzi kote Australia Jumanne, Waziri Mkuu Anthony Albanese alisema serikali imefanya mabadiliko haya ili kusaidia watoto wanaokua wakikabiliwa na algorithimu, mitiririko isiyoisha ya taarifa za mitandao ya kijamii na shinikizolinalotokana nao. Pia aliwahimiza watoto kucheza michezo, muziki, kusoma vitabu, na kufurahia muda wa ana kwa ana pamoja na familia na marafiki kwenye likizo za shule.

Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Usalama Mtandaoni (Umri wa chini kabisa kwa mitandao ya kijamii) wa Mwaka 2024 (Online Safety Amendment (Social Media Minimum Age) Bill 2024) ilipitishwa Novemba ya mwaka huu, ikiwataka majukwaa husika ya mitandao ya kijamii kuchukua “hatua zinazofaa”. Majukwaa yasiyotekeleza sheria hiyo yatatozwa faini ya hadi Dola za Australia milioni 49.5 (takriban Dola za Marekani milioni 32.8).

Uchunguzi wa hivi karibuni unaonyesha kwamba 73% ya wananchi wanaunga mkono marufuku hii, hasa kwa walimu na wazazi. Lakini asilimia 26 tu wanaamini hatua hii itafanikiwa.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha