Idadi ya watu waliofariki baada ya majengo mawili kuporomoka nchini Morocco yafikia 22

(CRI Online) Desemba 11, 2025

Idadi ya watu waliofariki baada ya majengo mawili ya makazi kuporomoka mjini Fez, Morocco, imeongezeka na kufikia 22.

Mamlaka nchini humo zimesema, tukio hilo limetokea jumanne jioni katika eneo la Al-Mustaqbal baada ya jengo lililokuwa tupu kuporomoka, na kusababisha jengo lililokuwa jirani la ghorofa nne, ambako sherehe ya kuzaliwa mtoto ilikuwa ikifanyika, kuporomoka.

Mamlaka zinasema, watu 11 wamejeruhiwa katika tukio hilo, huku wengine wakiwa na hali mbaya, na kwamba waathirika wengi ni wanawake na watoto.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha