Lugha Nyingine
Kundi la M23 la DRC ladai kuteka mji wa Uvira
(CRI Online) Desemba 11, 2025
Kundi la waasi la M23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), limedai kuudhibiti mji wa Uvira, ambao ni wa kimkakati katika jimbo la Kivu, kusini mashariki mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Radio Okapi nchini DRC jana, wapiganaji wa kundi hilo waliingia katika mji wa Uvira jana asubuhi. Msemaji wa kundi hilo Bw. Lawrence Kanyuka amesema kupitia mtandao wa kijamii kwamba, mji wa Uvira umekombolewa na kundi hilo.
Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kwamba, Burundi imefunga mpaka wake na DRC kutokana na hali ya sasa huko Uvira.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



