Uzalishaji na uuzaji wa magari nchini China kutoka Januari hadi Novemba wazidi milioni 31

(CRI Online) Desemba 12, 2025

Picha iliyopigwa Novemba 3, 2025 ikionesha mstari mpya wa uzalishaji wa magari yanayotumia nishati mpya (NEV) wa BYD, kampuni ongozi ya magari ya NEV wa China, kwenye kiwanda cha BYD mjini Zhengzhou, Mkoani Henan, China. (Xinhua/Li Jianan)

Picha iliyopigwa Novemba 3, 2025 ikionesha mstari mpya wa uzalishaji wa magari yanayotumia nishati mpya (NEV) wa BYD, kampuni ongozi ya magari ya NEV wa China, kwenye kiwanda cha BYD mjini Zhengzhou, Mkoani Henan, China. (Xinhua/Li Jianan)

Takwimu zilizotolewa na Shirikisho la Viwanda vya Magari la China Alhamisi zimeonesha kuwa, viwanda vya magari vya China vimedumisha mwelekeo mzuri wa kuongezeka, huku uzalishaji na uuzaji vimezidi magari milioni 31 kila mmoja katika miezi 11 ya kwanza mwaka huu.

Katika kipindi cha Januari hadi Novemba, uzalishaji wa magari wa China umeongezeka kwa asilimia 11.9 ukilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, na kufikia zaidi ya magari milioni 31.23. Na uuzaji wa magari umefikia karibu milioni 31.13, ongezeko la asilimia 11.4 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.

Mwezi Novemba pekee, uzalishaji na uuzaji wa magari wa China ulifikia milioni 3.532 na milioni 3.429 mtawalia, ukidumisha mwelekeo wa ongezeko thabiti.

Katika kipindi cha Januari hadi Novemba, uzalishaji na uuzaji wa magari yanayotumia nishati mpya (NEVs) ya China ulifikia milioni 14.907 na milioni 14.78 mtawalia, na kuongezeka kwa asilimia 31.4 na asilimia 31.2 ukilinganishwa na mwaka uliopita.

Ofisa wa shirikisho hilo Chen Shihua alisema, uzalishaji na uuzaji wa magari wa China unakadiriwa kufikia rekodi mpya ya juu mwaka 2025, kutokana na hatua za kisera, mahitaji ya ndani yanayoongezwa na uhimilivu mkubwa wa biashara ya nje.

Chen alisema uuzaji wa nchi za nje wa magari ya China ulifikia milioni 6.343 katika miezi 11 ya kwanza mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha