Uimbaji wa kusimulia ya Yimakan wa Kabila la Wahezhe wa China waongezwa na UNESCO kwenye Orodha ya Mali ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika wa Binadamu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 12, 2025

Video hii ikionyesha mafanyikio yaliyopatikana ya kuhifadhi “Uimbaji wa kusimulia wa Yimakan wa Kabila la Wahezhe la China” kwenye mkutano wa 20 wa kawaida wa Kamati ya Serikali ya Kuhifadhi Mali ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika mjini New Delhi, India, Desemba 11, 2025. (Xinhua/Wu Yue)

NEW DELHI — Kamati ya Kiserikali ya Kuhifadhi Mali ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika ya UNESCO, katika mkutano wa 20 wa kawaida, imeamua kuihamisha “Uimbaji wa kusimulia wa Yimakan wa Kabila la Wahezhe” wa China kutoka Orodha ya Mali ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika ambao unahitaji uhifadhi wa dharura hadi kwenye Orodha ya Wawakilishi wa Mali ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika wa Binadamu.

Wakati huo huo, kamati hiyo imeamua kuingiza mpango wa uhifadhi wa uimbaji wa Yimakan katika Orodha ya Utendaji Mzuri wa Uhifadhi. Hii ni mara ya kwanza kwa China kufanikisha kwa wakati mmoja kuifanya mali ya urithi wa uhifadhi kuhamishwa kwenye orodha moja na kuingizwa kwenye Orodha ya Utendaji Mzuri wa Uhifadhi.

Uimbaji wa kusimulia wa Yimakan ni uimbaji wa jadi wa kusimulia kwa mdomo wa Kabila la Wahezhe wenye historia ndefu na kurithishwa kizazi baada ya kizazi. Uimbaji huu unasimulia historia ya kabila hilo, hadithi za mashujaa, maisha ya uvuvi na uwindaji, mila na desturi, na maadili ya kabila la Wahezhe.

Mpaka sasa, miradi ya China iliyowekwa kwenye Orodha na Kumbukumbu husika za Mali ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika ya UNESCO imeongezeka na kuwa 45 kwa jumla.

Video hii ikionyesha mafanyikio yaliyopatikana ya kuhifadhi “Uimbaji wa kusimulia wa Yimakan wa Kabila la Wahezhe la China” kwenye mkutano wa 20 wa kawaida wa Kamati ya Kiserikali ya Kuhifadhi Mali ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika mjini New Delhi, India, Desemba 11, 2025. (Xinhua/Wu Yue)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha