Marekani yapanga kuchukua mafuta kutoka meli zilizokamatwa karibu na bahari ya karibu na Venezuela

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 12, 2025

Katibu wa Habari wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt, akihudhuria kwenye mkutano wa kila siku na waandishi wa habari mjini Washington, D.C., Marekani, Des. 11, 2025. (Picha na Li Yuanqing/Xinhua)

WASHINGTON — Katibu wa Habari wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt, alisema Alhamisi kuwa Marekani inapanga kuchukua mafuta kwenye meli ya mafuta ambayo jeshi la Marekani liliikamata Jumatano kwenye eneo karibu na pwani ya Venezuela.

Vyombo vingi vya habari vilinukuu maneno ya maofisa wa Ikulu ya White House na kuripoti jana Alhamisi kuwa, katika wiki kadhaa zijazo, serikali ya Trump inaweza kuchukua hatua nyingine zinazofanana kwa meli za mafuta zilizowekwa vikwazo katika eneo karibu na Venezuela. Leavitt alikataa kutoa maelezo kuhusu vitendo vya baadaye vya Ikulu ya White House.

Leavitt alisema katika mkutano na waandishi wa habari wa Ikulu ya White House kwamba, "Meli hii iliyowekwa vikwazo inabeba mafuta kutoka soko la magendo na kuyasafirisha mafuta kwa IRGC (Jeshi la Mapinduzi la Uislamu) ambalo liliwekwa vikwazo pia," alisema Leavitt.

Katika miezi minne iliyopita, Marekani imeweka vikosi vingi vya kijeshi katika eneo la Bahari ya Karibiani, vingi zaidi kati yao vimewekwa kwenye maeneo yaliyoko karibu na bahari ya Venezuela. Upande wa Marekani unadai kuwa hatua hii ni kupiga pigo dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya — Venezuela imeyalaani maneno hayo kwamba hiki ni kisingizio cha kujaribu kupindua utawala wa Caracas.

Katibu wa Habari wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt, akihudhuria kwenye mkutano wa kila siku na waandishi wa habari mjini Washington, D.C., Marekani, Des. 11, 2025. (Picha na Li Yuanqing/Xinhua)

Katibu wa Habari wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt, akihudhuria kwenye mkutano wa kila siku na waandishi wa habari mjini Washington, D.C., Marekani, Des. 11, 2025. (Picha na Li Yuanqing/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha