Lugha Nyingine
Katibu mkuu wa UM aeleza wasiwasi kuhusu mvutano unaozidi kuongezeka kati ya Marekani na Venezuela
(CRI Online) Desemba 12, 2025
Naibu msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq amesema Katibu Mkuu Antonio Guterres ameeleza wasiwasi kuhusu hali inayozorota ya mvutano kati ya Marekani na Venezuela, akitaka pande husika kujizuia na kuepuka kuchukua hatua zitakazoharibu utulivu wa Venezuela na wa kikanda.
Bw. Haq amesema Umoja wa Mataifa unataka pande husika zitekeleze wajibu wao kwa mujibu wa Katiba ya Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa.
Tarehe 10 mwezi huu, rais Donald Trump wa Marekani alisema jeshi la Marekani limekamata meli kubwa ya mafuta katika bahari karibu na Venezuela huku waziri wa mambo ya nje wa Venezuela Yvan Gil akalaani kitendo hicho na kukidai kuwa “kitendo cha uharamia”.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



