Lugha Nyingine
Madagaska yazindua rasmi tume ya kitaifa ya mashauriano
(CRI Online) Desemba 12, 2025
Tume ya Kitaifa ya Mashauriano imezinduliwa rasmi jumatano wiki hii katika mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo.
Katika sherehe ya uzinduzi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughilikia Masuala ya Ujenzi Mpya, Hanitriniaina Razafimanantsoa amesema, Tume hiyo ni nguzo muhimu ya juhudi za ujenzi mpya wa nchi, ikilenga kuhakikisha ushiriki mpana wa umma.
Tume hiyo itadumu kwa miezi sita na itashirikisha ngazi zote kuanzia ngazi ya shina, kwa lengo la kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya katiba na kufanya maandalizi ya kuanzishwa kwa jamhuri ya tano.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



