Katibu mkuu wa UM aeleza wasiwasi kufuatia vurugu mashariki mwa DRC

(CRI Online) Desemba 12, 2025

Naibu msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema, Katibu Mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres ameeleza wasiwasi wake kufuatia kuongezeka kwa vurugu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) huku hali ya usalama ikizidi kuwa mbaya kuanzia Desemba 2.

Akizungumza jana, Farhan Haq amesema, Guterres analaani vikali mashambulio yanayofanywa na kundi la AFC lenye ushirika na kundi la waasi la M23 katika maeneo kadhaa mkoa wa Kivu Kusini, ikiwemo Kamanyola, Luvungi, Katogota na Uvira, na kusababisha vifo vya raia. Guterres ametoa wito wa kusitishwa mara moja na bila masharti kwa mapigano hayo.

Wito huo unatolewa wiki moja baada ya makubaliano ya amani yaliyoongozwa na Marekani kati ya Rwanda na DRC kusainiwa katika Ikulu ya White House ya Marekani.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha