Lugha Nyingine
Sudan Kusini yafikia makubaliano na pande zinazopingana nchini Sudan juu ya eneo muhimu la mafuta
(CRI Online) Desemba 12, 2025
Sudan Kusini imesema imefikia makubaliano na pande zinazopingana nchini Sudan ili kukomboa eneo la mafuta la Heglig, baada ya eneo hilo kudhibitiwa na Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF).
Waziri wa Habari, Teknolojia ya Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Ateny Wek Ateny amewaambia wanahabari mjini Juba, kwamba makubaliano ya pande tatu yalifikiwa na Jeshi la Ulinzi la Sudan Kusini, Jeshi la Ulinzi la Sudan, na kikosi cha RSF.
Hatua hiyo imekuja baada ya kikosi cha RSF kusema jumatatu wiki hii, kwamba kimechukua udhibiti kamili wa eneo la kuzalisha mafuta la Heglig mkoa wa Kordofan Kusini kufuatia jeshi la serikali kuondoka eneo hilo.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



