Lugha Nyingine
Maofisa wa AU wataka hatua za dharura zichukuliwe kukabiliana na umasikini wa nishati barani Afrika
Maofisa wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) wametoa wito wa hatua za dharura zichukuliwe ili kukabiliana na umasikini mkali wa nishati unaowakabili watu wengi katika eneo la Afrika kusini mwa Sahara.
Wito huo umetolewa katika Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri wa Ufanisi wa Nishati Afrika, ulioanza jumatano wiki hii katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, kwa lengo la kupunguza matumizi makubwa ya nishati kuliko inavyotakiwa na kutuliza mifumo ya nishati katika bara hilo.
Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf amesema, ufanisi wa nishati ni mstari wa kwanza wa ulinzi dhidi ya umasikini wa nishati, wenye uwezo wa kuboresha uzalishaji na kupunguza gharama za nishati, na kutoa wito wa kuchukuliwa hatua za dharura ili kukabiliana changamoto tatu za usalama wa nishati, gharama nafuu, na maingiliano ya kikanda.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



