Lugha Nyingine
China yaihimiza jumuiya ya kimataifa kuzisaidia nchi za Afrika ya kati kuongeza uwezo wao wa kujilinda
Naibu mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Sun Lei jana ameihimiza jumuiya ya kimataifa izisaidie nchi za Afrika ya kati ka kuongeza uwezo wao wa kujilinda.
Balozi Sun amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kushikilia maoni ya pamoja ya usalama, ujumuishi, ushirikiano na uendelevu, na kuongeza msaada katika ufahamu wa hali ya usalama, uwekezaji wa fedha, na taarifa za matishio ili kuzisaidia nchi za Afrika ya kati kuimarisha uwezo wao wa kujilinda, na kuimarisha mstari wa usalama wa eneo hilo.
Balozi Sun pia amesema, jumuiya ya kimataifa inapaswa kutoa msaada wa kiujenzi katika ufadhili wa uchaguzi, ujumuishaji na usuluhishi na mageuzi ya taasisi, kulingana na mazingira maalum ya nchi za eneo hilo, ili kuweka msingi imara kwa nchi hizo kuhimiza mchakato wa siasa na amani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



