Lugha Nyingine
Rais wa Afrika Kusini asisitiza ahadi ya SADC kwa amani na utulivu wa kikanda
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesisitiza tena ahadi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) katika kuhimiza amani, usalama na utulivu wa kisiasa kwenye eneo hilo, kupitia utekelezaji wa Itifaki ya SADC juu ya Siasa, Ulinzi na Ushirikiano wa Usalama.
Akizungumza jana Jumatano kwa nafasi yake ya mwenyekiti wa muda wa SADC kwenye mkutano maalum wa viongozi wa SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao, Rais Ramaphosa amesema ingawa hatua imepigwa katika kusukuma mbele amani na utulivu, changamoto za kisiasa na usalama zinaendelea kuathiri sehemu za eneo hilo.
Rais Ramaphosa ameonyesha wasiwasi hasa kuhusu hali ya usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, akiielezea kuwa ni jambo linalotia "wasiwasi mkubwa," na ametoa wito wa juhudi endelevu za kikanda ili kurejesha utulivu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



