Mkutano wa 6 wa Baraza la Vyombo vya Habari la China na Russia lalenga kuunga mkono maendeleo ya nchi zote mbili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 18, 2025

Li Shulei, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC, akihudhuria na kuhutubia Mkutano wa 6 wa Baraza la Vyombo vya Habari la China na Russia mjini Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 16, 2025. (Xinhua/Jin Liangkuai)

BEIJING - Mkutano wa sita wa Baraza la Vyombo vya Habari la China na Russia, lililofanyika mjini Beijing jana Jumanne, lilijadili njia za kuhimiza urafiki na kuunga mkono maendeleo ya nchi hizo mbili kupitia ushirikiano wa vyombo vya habari.

Li Shulei, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC, alihudhuria na kuhutubia mkutano huo.

Wahudhuriaji wamesema kwamba chini ya mwongozo wa kimkakati wa wakuu wa nchi hizo mbili, uhusiano kati ya China na Russia umeendelea kudumisha maendeleo thabiti, mazuri na ya kiwango cha juu, na kuunda mfano wa aina mpya ya uhusiano wa kimataifa na uhusiano kati ya nchi kubwa jirani.

Mwezi Mei mwaka huu, wakuu wa nchi hizo mbili walisaini na kutoa taarifa ya pamoja kuhusu kuzidisha uhusiano na ushirikiano wa kimkakati wa pande zote wa uratibu katika zama mpya kati ya China na Russia, na kupendekeza waziwazi kuimarisha ushirikiano katika sekta ya vyombo vya habari kati ya nchi hizo mbili.

"Sekta za vyombo vya habari za China na Russia zinapaswa kutekeleza kikamilifu makubaliano hayo muhimu yaliyofikiwa kati ya wakuu wa nchi hizo mbili, kufuata bila kuyumba mwelekeo wa jumla wa urafiki kati ya China na Russia, na kujenga mazingira chanya ya maoni ya umma kwa ajili ya maendeleo ya pamoja ya China na Russia," wahudhuriaji wamesema.

Pia wamesema kwamba vyombo vya habari vya nchi hizo mbili vinapaswa kutilia maanani masuala makubwa kama vile kuratibiwa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa China na mikakati ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Russia, na kutoa ripoti za kina juu ya mafanikio ya ushirikiano wa kunufaishana katika sekta mbalimbali.

Wamesema kuwa vyombo vya habari vinapaswa kujenga madaraja ya muunganisho wa watu, kuhimiza mawasiliano na kufunzana kati ya ustaarabu wa China na Russia, kuungana mkono kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya kidijitali na AI, na kufanya kazi pamoja ili kuongeza ushawishi wa vyombo vya habari.

Baraza hilo limeandaliwa na Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC na Ofisi ya Utendaji ya Rais ya Russia, na kuratibiwa na Shirika la Habari la China, Xinhua na Shirika la Habari la Russia, TASS.

Takriban maafisa na wawakilishi wa vyombo vya habari 140 kutoka nchi zote mbili walihudhuria mkutano huo, ambapo pande hizo mbili zilisaini nyaraka 11 juu ya kuimarisha ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya China na Russia.

Picha hii iliyopigwa Desemba 16, 2025 ikionyesha Mkutano wa 6 wa Baraza la Vyombo vya Habari la China na Russia uliofanyika Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Zhang Chenlin)

Picha hii iliyopigwa Desemba 16, 2025 ikionyesha Mkutano wa 6 wa Baraza la Vyombo vya Habari la China na Russia uliofanyika Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Zhang Chenlin)

Wageni waalikwa wakihudhuria Mkutano wa 6 wa Baraza la Vyombo vya Habari la China na Russia uliofanyika Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 16, 2025. (Xinhua/Zhou Tinglu)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha