Waasi wa M23 waanza kuondoka kutoka Uvira mashariki mwa DRC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 18, 2025

Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha askari wa kundi la waasi la Vuguvugu la Machi 23 (M23) wakitembea mjini Uvira, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Desemba 17, 2025. (Picha na Alain Uaykani/Xinhua)

UVIRA, DRC - Wapiganaji kutoka kundi la waasi la Vuguvugu la Machi 23 (M23) jana Jumatano walianza kuondoka kutoka kwenye nafasi zao katika Mji wa Uvira, mji wa kimkakati mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la China, Xinhua ameshuhudia akiwa maeneo husika.

"Mjongeo wa vikosi vya AFC/M23 kutoka mji wa Uvira unaendelea na utakamilika ifikapo kesho (leo Alhamisi)," kiongozi wa kisiasa wa M23 Bertrand Bisimwa ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, akitoa wito wa kuwataka wakazi wa huko wawe na tulivu.

Magari ya kijeshi na askari wa M23 walionekana wakiondoka kutoka kwenye kambi yao kuu katika mji huo. Lawrence Kanyuka, msemaji wa kundi hilo la waasi, amethibitisha kuondoka kwa waasi hao lakini hakutoa maelezo zaidi.

Baada ya kudai Desemba 10 kuwa limeuteka mji huo wa Uvira, Kundi la M23 lilitangaza uamuzi wake Jumatatu wiki hii wa "kuondoa vikosi vyake kwa upande mmoja" kufuatia ombi la wapatanishi wa Marekani.

Corneille Nangaa, kiongozi wa Muungano wa Mto Congo (AFC), muungano wa kisiasa na kijeshi unaoshirikiana na M23, amesisitiza kuondoka kwa "masharti", akihimiza mahakikisho ya usalama, ikiwa ni pamoja na kupelekwa kwa kikosi kisichopendelea upande wowote.

Katika taarifa yake Jumatatu jioni, Nangaa alisema kwamba uamuzi huo umefuatia upigaji hatua wa hivi karibuni kwenye mchakato wa amani wa Doha, ikiwa ni pamoja na kusainiwa kwa Makubaliano ya Doha mwezi Novemba.

Mji huo wa Uvira, uko karibu na mpaka wa Burundi kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika, ulikuwa kituo cha mambo ya utawala cha muda cha Jimbo la Kivu Kusini baada ya mji mkuu Bukavu wa jimbo hilo kushikiliwa na M23 mwezi Februari.

Wachambuzi na watu waletao habari wa eneo hilo wameonya kwamba kuipoteza Uvira baada ya muda kunaweza kufungua njia kuelekea kusini-mashariki mwa DRC, ikiwa ni pamoja na Haut-Katanga, eneo muhimu la kiuchumi. Mapigano pia yameripotiwa katika maeneo yaliyo kusini zaidi ya Baraka na Fizi ya Jimbo la Kivu Kusini.

Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha askari wa kundi la waasi la Vuguvugu la Machi 23 (M23) wakitembea mjini Uvira, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Desemba 17, 2025. (Picha na Alain Uaykani/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha askari wa kundi la waasi la Vuguvugu la Machi 23 (M23) wakitembea mjini Uvira, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Desemba 17, 2025. (Picha na Alain Uaykani/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha askari wa kundi la waasi la Vuguvugu la Machi 23 (M23) wakitembea mjini Uvira, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Desemba 17, 2025. (Picha na Alain Uaykani/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha askari wa kundi la waasi la Vuguvugu la Machi 23 (M23) wakitembea mjini Uvira, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Desemba 17, 2025. (Picha na Alain Uaykani/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha