Lugha Nyingine
Mfumuko wa bei wa watumiaji wa Afrika Kusini wapungua hadi asilimia 3.5 mwezi Novemba

Mteja akifanya manunuzi kwenye supamaketi jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Desemba 17, 2025. (Xinhua/Chen Wei)
JOHANNESBURG – Takwimu zilizotolewa jana Jumatano na shirika la Afrika Kusini (Stats SA) zimeonesha kuwa, mfumuko wa bei wa watumiaji wa Afrika Kusini ulipungua kidogo hadi asilimia 3.5 mwezi Novemba kutoka asilimia 3.6 mwezi Oktoba, ambapo usafiri barabarani, burudani, michezo, na utamaduni, vilevile na upashanaji wa habari na mawasiliano, vilikuwa vichangiaji vikuu vya kushuka kwa kasi kwa mfumo huo, amesema Patrick Kelly, mkurugenzi mkuu wa takwimu za bei wa Stats SA.
"Kiwango cha mabadiliko ya mwaka ya usafiri barabarani kilishuka hadi asilimia 0.7 mwezi Novemba kutoka asilimia 1.5 mwezi Oktoba. Mfumuko wa bei wa magari ulikuwa asilimia 0.9, ukifikia kiwango cha chini kabisa tangu Juni 2013 wakati kiwango hicho pia kilipokuwa asilimia 0.9," amesema Kelly, akiongeza kuwa bei za mafuta zilishuka kwa asilimia 2.2 kati ya Oktoba na Novemba, na kuufanya mfumuko wa mafuta wa mwaka kufikia hadi asilimia 0.1.
Shirika hilo la takwimu la Afrika Kusini (Stats SA), limesema mfumuko wa bei wa chakula uliongezeka hadi asilimia 4.4 mwezi Novemba kutoka asilimia 3.9 mwezi Oktoba, huu ni ongezeko lake la kwanza katika miezi minne. Limesema, mfumuko wa bei wa vinywaji visivyo na kileo, migahawa na huduma za malazi, vilevile wa vinywaji vyenye kileo na tumbaku, uliongezeka zaidi mwezi Novemba.
"Bei za nyama ziliongezeka kwa wastani wa asilimia 12.2 katika miezi 12 hadi Novemba, na kufikia kiwango cha juu zaidi cha mwaka tangu Januari 2018. Kushuka kwa bei za maziwa, mayai, na bidhaa nyingine za maziwa kuliendelea kwa mwezi wa sita mfululizo," Kelly amesema.

Mteja akifanya manunuzi kwenye supamaketi jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Desemba 17, 2025. (Xinhua/Chen Wei)

Wateja wakichagua bidhaa kwenye supamaketi jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Desemba 17, 2025. (Xinhua/Chen Wei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



