Lugha Nyingine
Rais wa Uganda aahidi uchaguzi mkuu huru na wa haki
(CRI Online) Desemba 19, 2025
Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameahidi kuwa uchaguzi mkuu ujao wa Uganda utakuwa huru na wa haki, huku akihimiza wapiga kura kujitokeza kwa wingi.
Rais Museveni, ambaye anatafuta kuchaguliwa tena kwa muhura mwingine, amesema hayo jana Alhamisi alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Wilaya ya Rakai, Mkoa wa Kati wa Uganda, ikiwa ni sehemu ya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu huo.
Rais Museveni amesema kudumisha amani kunaendelea kuwa kipaumbele cha juu cha serikali, na pia ni msingi wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi hiyo.
(Wahariri wa tovuti:Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



