UN yasema raia zaidi ya 1,000 waliuawa katika shambulizi la Aprili la RSF dhidi ya kambi ya wakimbizi nchini Sudan

(CRI Online) Desemba 19, 2025

Picha hii inamwonesha Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Beirut, Lebanon, Januari 16, 2025. (Xinhua/Bilal Jawich)

Picha hii inamwonesha Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Beirut, Lebanon, Januari 16, 2025. (Xinhua/Bilal Jawich)

Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa jana Alhamisi inasema kuwa watu zaidi ya 1,000 waliuawa katika siku tatu za mashambulizi yaliyofanywa mwezi Aprili na kundi la wanamgambo wa Vikosi vya Uungaji Mkono wa Haraka (RSF) dhidi ya kambi ya wakimbizi ya Zamzam katika Jimbo la Darfur Kaskazini.

“Angalau raia 1,013 waliuawa wakati wa mashambulizi hayo kuanzia Aprili 11 na 13,” ripoti hiyo kutoka Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa (OHCHR) imesema, ikionyesha "mtindo unaoendelea" wa ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu na ukandamizaji mkubwa wa haki za binadamu.

Ripoti hiyo inasema, miongoni mwa waliouawa, 319 waliuawa bila hatia,ama wakiwa ndani ya kambi au wakati wakijaribu kukimbia. Imesema wengine waliuawa katika nyumba zao wakati wa ukaguzi wa nyumba kwa nyumba, na pia kwenye soko kuu, shule, vituo vya afya, na misikitini.

(Wahariri wa tovuti:Renato Lu)

Picha