Afrika Kusini yatetea operesheni yake ya uhamiaji, yakataa madai ya Marekani huku mvutano kati yao ukipamba moto

(CRI Online) Desemba 19, 2025

Afrika Kusini imetetea operesheni yake ya uhamiaji iliyosababisha kufukuzwa kwa raia saba wa Kenya, ikikataa madai ya Marekani ya kuwatendea kinyume cha utaratibu maofisa wa Marekani.

Katika taarifa iliyotolewa jana Alhamisi na Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Ushirikiano ya Afrika Kusini (DIRCO), serikali ya Afrika Kusini imesema kufukuzwa kwa raia hao saba wa Kenya na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afrika Kusini (DHA) kulitekelezwa kwa kufuata kikamilifu sheria za uhamiaji za nchi hiyo.

“Watu hao walibainika kufanya kazi bila kuwa na vibali vya kazi vinavyohitajika, kinyume cha kanuni za uhamiaji,” imesema, ikiongeza kuwa Afrika Kusini haitajadiliana juu ya mamlaka na utekelezaji wake wa utawala wa sheria.

Baadhi ya vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa wafanyakazi wawili wa Marekani “walishikiliwa kwa muda na kuachiwa” wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha