China na Zimbabwe zasaini makubaliano ya kuboresha miundombinu ya umwagiliaji

(CRI Online) Desemba 19, 2025

China na Zimbabwe zimesaini makubaliano jana Alhamisi kuhusu mradi wa maboresho na ukarabati wa skimu za umwagiliaji zilizofadhiliwa na China, ambao unalenga kuimarisha tija ya kilimo na uhimilivu wa mabadiliko ya tabianchi wa Zimbabwe.

Kwa mujibu wa Ubalozi wa China nchini Zimbabwe, mradi huo utaboresha na kukarabati vituo tisa vya umwagiliaji katika majimbo sita ya Zimbabwe.

Akijibu swali kutoka Shirika la Habari la China, Xinhua baada ya hafla ya utiaji saini, Waziri wa Fedha wa Zimbabwe Mthuli Ncube amesema uungaji mkono huo kutoka China utawezesha kufikiwa kwa lengo la Zimbabwe la kuongeza ardhi ya umwagiliaji na kuboresha kilimo ili kuongeza tija, hasa kwa wakulima wa vijijini.

“Mradi huu wa umwagiliaji pia utasaidia kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha usalama wa chakula, kwani kilimo kinachotegemea mvua kiko katika hatari ya kuathiriwa na matatizo ya tabianchi kama vile ukame na mvua zisizotabirika.” Ncube ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha