Lugha Nyingine
Tovuti ya Gazeti la Umma yafanya "Usiku wa AI mjini Xi'an," kuonyesha mustakabali wa tasnia ya habari unaowezeshwa na AI

"Kuafu", roboti ya AI, ikitumbuiza tai chi na wanafunzi jukwaani. (Poeple's Daily Online/Zou Xing)
"Usiku wa AI mjini Xi'an," shughuli iliyoonesha teknolojia za hali ya juu za AI za China na matumizi yake katika maisha halisi, imefanywa na Tovuti ya Gazeti la Umma (People's Daily Online) Desemba 18 katika Mji wa Xi'an, mji mkuu wa Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China, mji ambao utamaduni wa jadi na teknolojia ya kisasa vinaishi pamoja kwa mapatano.
Shughuli hiyo iliwaleta pamoja wawakilishi wa kampuni, wataalamu na wasomi kutoka maeneo mbalimbali ya tasnia ya AI. Kupitia muunganiko changamani wa sanaa na teknolojia, uliowasilishwa katika muundo wa kidijitali wa siku za baadaye, shughuli hiyo ilionyesha dhahiri mafanikio ya teknolojia mpya za kisasa na mambo mapya ya kiteknolojia katika AI.
Shughuli hiyo pia ilihusu tukio la kusainiwa kwa makubaliano ya kuanzisha Kituo cha Ushirikiano wa Elimu na Matumizi ya AI "Dreamland" kati ya Chuo Kikuu cha Xi'an Jiaotong na Tovuti ya Gazeti la Umma.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



