Uwanja mkubwa zaidi wa mafuta wa baharini wa China waripoti uzalishaji wa mwaka wa mafuta na gesi wa kuvunja rekodi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 22, 2025

BEIJING - Uwanja mkubwa zaidi wa mafuta wa bahariniwa China, Uwanja wa Mafuta wa Bohai, umezalisha zaidi ya tani milioni 40 za mafuta na gesi kwa kipimo sawa cha mafuta mwaka 2025, na kuweka rekodi mpya ya kihistoria, Shirika la Taifa la Mafuta ya Baharini la China (CNOOC) limetangaza jana Jumapili.

Ukiwa ni Uwanja unaongoza wa mafuta wa baharini nchini China kwa kiwango na uzalishaji, uzalishaji huo wa kuvunja rekodi utatoa uungaji mkono thabiti kwa usalama wa nishati wa China na maendeleo ya kiuchumi na kijamii yenye sifa bora, kwa mujibu wa CNOOC.

CNOOC imesema uwanja huo wa Mafuta wa Bohai, kwa sasa unaendesha zaidi ya maeneo 60 ya uzalishaji wa mafuta na gesi, huku uzalishaji wake wa jumla wa mafuta ghafi ukizidi tani milioni 600. Na katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, uzalishaji wake wa mafuta na gesi umeendelea kuongezeka kwa asilimia 5 kwa mwaka.

Kampuni pia hiyo imesema kwamba Uwanja wa Mafuta wa Bohai unaendelea kusukuma mbele mageuzi ya kidijitali na ya kijani, na mafanikio yamepatikana katika ujanibishaji wa vifaa muhimu, ikiwemo kufungwa kwa mfumo wa kwanza wa uzalishaji chini ya bahari katika kina kifupi cha maji uliotengenezwa nchini China. Wakati huo huo, zaidi ya asilimia 80 ya maeneo ya uzalishaji katika Uwanja wa Mafuta wa Bohai yameunganishwa na vyanzo vya umeme vya nchi kavu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha