Uwekezaji wa China waimarisha ujanibishaji wa viwanda wa Misri huku uhusiano wa pande mbili ukizidi kuimarika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 22, 2025

Picha hii ya kumbukumbu isiyo na tarehe ikionyesha mandhari ya Eneo Maalum la Ushirikiano wa Kiuchumi na Biashara kati ya China na Misri la TEDA Suez katika Wilaya ya Ain Sokhna ya Jimbo la Suez, Misri. (TEDA Investment Holding/kupitia Xinhua)

CAIRO - Uwekezaji wa China unaozidi kuongezeka nchini Misri unasaidia nchi hiyo ya Kiarabu kuunda upya muundo wake wa viwanda, kwa kuhamisha mwelekeo kutoka utegemezi wa biashara kuelekea uzalishaji wa viwanda vilivyojanibishwa na vinavyolenga mauzo ya nje, huku uhusiano wa pande mbili ukiendelea kuimarika.

Katika miaka ya hivi karibuni, uwekezaji wa China nchini Misri umeendelea kujikita zaidi katika ujenzi wa viwanda na upanuzi wa shughuli za uzalishaji, ukiunga mkono juhudi za Misri za kujanibisha uzalishaji, kuimarisha viwanda vya thamani iliyoongezwa, na kujiweka kama kituo cha uzalishaji wa viwanda cha kikanda wakati ambapo kuna hali ya kutokuwa na uhakika ya biashara duniani.

Duru za wafanyabiashara za Misri zinaona mabadiliko hayo kuwa ni kiashiria muhimu cha kuongezeka kwa kina cha ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya Misri na China.

"Misri inalenga kutimiza ujanibishaji wa viwanda. Baadhi ya nchi huwekeza nchini Misri kwa kununua viwanda, jambo ambalo ni uhamishaji wa umiliki, badala ya uwekezaji wa kweli, lakini China inakuja kujenga viwanda halisi," amesema Mostafa Ibrahim, makamu mwenyekiti wa kamati ya China katika Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Misri.

Ibrahim ameongeza kuwa upanuzi wa miradi ya China nchini Misri unaonyesha nguvu ya sasa ya uhusiano wa pande mbili wa kiuchumi na kisiasa, ambao kwa sasa uko "katika kilele chake."

Hassan El-Khatib, Waziri wa Uwekezaji na Biashara ya Nje wa Misri, amesema awamu inayofuata ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Misri na China inapaswa kutilia mkazo katika kupanua uzalishaji wa pamoja na kuimarisha viwanda vya ndani vinavyolenga mauzo ya nje.

Ameelezea kwamba Dira ya maendeleo endelevu ya Misri ya 2030 inaendana kwa karibu na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja la China, hasa katika maeneo yanayohusiana na mafungamano ya kikanda, muunganisho wa viwanda, na biashara ya kuvuka mipaka. Amesisitiza kuwa, nafasi ya kimkakati kijiografia ya Misri inayounganisha mabara matatu, gharama za ushindani za nguvukazi, na mikataba mipana ya biashara inayowezesha ufikiaji wa masoko ya dunia.

Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye mstari wa uzalishaji wa nyuzi za vioo (fiberglass) kwenye kiwanda cha kampuni kubwa ya nyuzi za vioo ya China, Jushi katika Eneo Maalum la Ushirikiano wa Kiuchumi na Biashara kati ya China na Misri la TEDA Suez katika wilaya ya Ain Sokhna ya Jimbo la Suez, Misri, Novemba 6, 2024. (Xinhua/Ahmed Gomaa)

Sehemu kubwa ya msukumo huo wa viwanda vilivyojanibishwa unajitokeza ndani ya majukwaa yaliyoteuliwa ya viwanda ya Misri, haswa Eneo Maalum la Kiuchumi la Mfereji wa Suez (SCZone), ambalo limeibuka kuwa kituo kikuu cha uwekezaji wa viwanda wa China.

Katika kipindi cha miaka mitatu na nusu iliyopita, Eneo hilo la SCZone limevutia uwekezaji wa jumla wa dola bilioni 11.6 za Marekani, huku wawekezaji wa China wakichukua takriban asilimia 50 ya jumla hiyo, kwa mujibu wa Waleid Gamal El-Dein, mwenyekiti wa mamlaka ya Eneo la SCZone.

El-Dein amesisitiza umuhimu wa Eneo Maalum la Ushirikiano wa Kiuchumi na Biashara kati ya China na Misri la TEDA Suez ndani ya Eneo hilo la SCZone, akisema kuwa kwa sasa linajumuisha zaidi ya miradi 200 ya viwanda, huduma, na uchukuzi, yenye jumla ya uwekezaji wa takriban dola bilioni 3.8 za Marekani.

Mfanyakazi Mchina akionekana kwenye eneo la ujenzi wa Eneo la Kati la Biashara (CBD) la mji mkuu mpya wa kiutawala wa Misri, kilomita 45 mashariki mwa Cairo, Misri, Novemba 22, 2023. (Xinhua/Sui Xiankai)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha