Wajasiriamali wanawake wa Ethiopia wahitimu mafunzo ya biashara yaliyoungwa mkono na China

(CRI Online) Desemba 22, 2025

Sun Mingxi, Kaimu Balozi wa Ubalozi wa China nchini Ethiopia, akizungumza kwenye sherehe ya mahafali ya warsha ya Mpango wa Uwezeshaji wa Ujasiriamali wa Wanawake Duniani (GFEEP) mjini Addis Ababa, Ethiopia, Desemba 20, 2025. (Xinhua/Liu Fangqiang)

Wajasiriamali wanawake zaidi ya 60 wa Ethiopia wamehitimu kutoka kwenye warsha ya Programu ya Uwezeshaji wa Ujasiriamali wa Wanawake Duniani (GFEEP) inayoungwa mkono na China mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia.

Wakati wa mafunzo hayo ya warsha ya wiki mbili, washiriki walihudhuria madarasa yaliyojikita katika mawazo ya kimkakati ya biashara, uelevu wa mambo ya kidijitali, mitindo ya biashara ya kisasa, na ujuzi muhimu wa kijasiriamali.

Akizungumza kwenye sherehe ya mahafali siku ya Jumamosi, Kaimu Balozi wa Ubalozi wa China nchini Ethiopia Sun Mingxi, amesema kuwa warsha hiyo ya mafunzo ni mpango halisi wa kujenga uwezo chini ya Mpango Kazi wa Mkutano wa Viongozi wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wa Beijing (2025-2027), unaolenga kuwezesha wanawake na kuhimiza usawa wa kijinsia barani Afrika.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyabiashara na Jumuiya za Kisekta za Ethiopia Tsedeke Digafe amesema warsha hiyo inaonyesha dhamira ya pamoja ya Ethiopia na China katika kuendeleza usawa wa kijinsia na kufikia Lengo la 5 la Maendeleo Endelevu la Umoja wa Mataifa.

Wanagenzi wakihudhuria sherehe ya mahafali ya warsha ya Mpango wa Uwezeshaji wa Ujasiriamali wa Wanawake Duniani (GFEEP) mjini Addis Ababa, Ethiopia, Desemba 20, 2025. (Xinhua/Liu Fangqiang)

Wanagenzi wakihudhuria sherehe ya mahafali ya warsha ya Mpango wa Uwezeshaji wa Ujasiriamali wa Wanawake Duniani (GFEEP) mjini Addis Ababa, Ethiopia, Desemba 20, 2025. (Xinhua/Liu Fangqiang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha