Viongozi wa Afrika watoa wito wa suluhisho linaloongozwa kikanda kwa mgogoro wa DRC

(CRI Online) Desemba 22, 2025

Viongozi wa Afrika jana Jumapili wametoa wito wa juhudi zinazoongozwa kikanda kuchukua kipaumbele katika kutatua mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), huku juhudi za kimataifa zikibeba jukumu la uungaji mkono.

Wito huo umetolewa kwenye mkutano wa viongozi wa kikanda wa siku moja uliofanyika mjini Entebbe nchini Uganda, ambao uliwaleta pamoja viongozi na wajumbe ili kushughulikia hali ya usalama inayozidi kuwa mbaya mashariki mwa DRC na kuenea katika eneo la Maziwa Makuu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda John Mulimba alisema washiriki wamekubaliana kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zinapaswa kuongoza juhudi za amani ili kushughulikia mgogoro huo unaozidi kupamba moto.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Vincent Biruta amesema hakukuwa na haja ya kuanzisha mifumo mipya ya kutatua mgogoro huo kwani changamoto kuu ipo katika ukosefu wa utekelezaji wa makubaliano ambayo tayari yamefikiwa.

Ameyaelezea makubaliano ya Washington na mipango ya amani ya Doha kuwa ni mifumo inayofaa zaidi ya kushughulikia mazingira yote ya ndani na ya kikanda ya mgogoro huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha