Ndege wa kuhamahama waonekana katika Ziwa Donggu mkoani Hunan, katikati mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 22, 2025
Ndege wa kuhamahama waonekana katika Ziwa Donggu mkoani Hunan, katikati mwa China
Picha hii iliyopigwa Desemba 16, 2025 ikionyesha ndege wa kuhamahama kwenye Ziwa Donggu katika Mji wa Yueyang, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China. (Picha na Zhou Yang/Xinhua)

Ziwa Donggu likiwa ni sehemu muhimu ya ukanda wa kiikolojia wa Ziwa Dongting katika Mji wa Yueyang, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, kila mwezi Novemba linakaribisha idadi kubwa ya ndege wa kuhamahama wanaotua kwenye ziwa hilo kwa ajili ya kushinda majira ya baridi.

Katika miaka ya hivi karibuni, miradi ya jumla ya ulinzi na urejesho wa ikolojia imekuwa ikifanywa katika eneo hilo. Juhudi hizo, ikiwa ni pamoja na kusafisha ziwa, kuongeza vyanzo vya chakula, na kurejesha mimea asilia ya huko, zimeboresha kwa udhahiri makazi ya ndege hao wa kuhamahama.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha