Lugha Nyingine
Xi Jinping atoa amri kuwapandishwa vyeo makamanda wawili kuwa majenerali

Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) Xi Jinping na viongozi wengine wakipiga picha pamoja na makamanda wawili waliopandishwa vyeo mjini Beijing, Desemba 22, 2025. (Xinhua/Li Gang)
BEIJING – Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) Xi Jinping, jana Jumatatu aliwakabidhi makamanda wawili vyeti vya amri ya kuwapandisha vyeo kuwa majenerali. Majenerali hao wawili waliopandishwa vyeo ni Yang Zhibin, Kamanda wa Eneo la Kivita la Mashariki la Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), na Han Shengyan, Kamanda wa Eneo Kuu la Kivita la PLA.
Zhang Youxia, Naibu Mwenyekiti wa CMC, alitangaza amri hiyo ya kuwapandisha vyeo, ambayo ilisainiwa na Xi Jinping, kwenye hafla ya kupandisha vyeo iliyofanyika mjini Beijing. Zhang Shengmin, Naibu Mwenyekiti wa CMC, aliongoza hafla hiyo.
Xi amewapongeza majenerali hao wawili.
Jenerali ni cheo cha juu zaidi kwa maofisa wa jeshini nchini China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



