China yasema Marekani kukamata kiholela meli ya nchi nyingine kunakiuka vibaya sheria ya kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 23, 2025

BEIJING -- Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian jana Jumatatu alipojibu swali la vyombo vya habari kuhusu Kikosi cha Walinzi wa Pwani cha Marekani kilikamata meli moja ya mafuta Desemba 20 kwa saa za Marekani alisema kuwa, kitendo cha Marekani cha kukamata kiholela meli ya nchi nyingine kimekiuka vibaya sheria ya kimataifa, huku ofisa wa Ikulu ya Marekani akidai kuwa meli hiyo ni cha kile kinachoitwa "meli ya kivuli (Shadow fleet) ".

"China siku zote inapinga vikwazo haramu vya upande mmoja ambavyo havina msingi katika sheria za kimataifa na havijaidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na pia inapinga vitendo vyovyote vinavyokiuka nia na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, kuvamia mamlaka ya nchi na usalama wa nchi nyingine, au vinavyokuwa vitendo vya kimabavu vya upande mmoja," Lin ameuambia mkutano na waandishi wa habari.

Lin ameongeza kuwa, Venezuela ina haki ya kujiendeleza kwa kujitawala na kufanya ushirikiano wa kunufaishana na nchi nyingine, na China inaamini kuwa jumuiya ya kimataifa inaelewa na kuunga mkono msimamo wa Venezuela katika kulinda haki na maslahi yake halali.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha