China yapata mafanikio thabiti katika uhifadhi wa ikolojia na mageuzi ya kijani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 23, 2025

Picha hii iliyopigwa Novemba 20, 2025 ikionyesha mandhari ya Ziwa Yamzbog Yumco katika Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China. (Xinhua/Li Jian)

Picha hii iliyopigwa Novemba 20, 2025 ikionyesha mandhari ya Ziwa Yamzbog Yumco katika Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China. (Xinhua/Li Jian)

BEIJING - China imepata maendeleo makubwa katika ulinzi wa ikolojia na mazingira wakati wa kipindi cha Mpango wake wa 14 wa Miaka Mitano (2021-2025), huku maboresho endelevu yakionekana katika sehemu mbalimbali.

Picha iliyopigwa Agosti 25, 2025 ikionyesha watalii wakitembelea sehemu ya Jinshanling ya Ukuta Mkuu katika Wilaya ya Luanping ya Mji wa Chengde, Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China. (Picha na Zhou Wanping/Xinhua)

China imechangia robo ya maeneo mapya ya kijani duniani tangu mwaka 2000, kiwango chake cha ueneaji wa misitu kimeongezeka hadi asilimia 25.09, kikionyesha maendeleo thabiti katika mipango mikubwa ya upandaji miti na urejeshaji wa ikolojia. Wakati huo huo, kiasi cha misitu nchini kimefikia mita za ujazo bilioni 20.99, kikifikia lengo la mwaka 2030 kabla ya wakati uliopangwa.

Ubora wa maji pia umeboreshwa kwa kiasi kikubwa. Mwaka 2024, asilimia 90.4 ya maeneo ya kitaifa ya ufuatiliaji wa maji ya juu ya ardhi yalifikia viwango bora vya ubora wa maji, na kuvuka asilimia 90 kwa mara ya kwanza.

Picha iliyopigwa Septemba 9, 2025 ikionyesha mandhari ya hifadhi ya mazingira ya asili ya ardhi oevu ya Xiaonanhai katika Mji wa Chongqing, kusini magharibi mwa China. (Xinhua/Tang Yi)

Picha iliyopigwa Septemba 9, 2025 ikionyesha mandhari ya hifadhi ya mazingira ya asili ya ardhi oevu ya Xiaonanhai katika Mji wa Chongqing, kusini magharibi mwa China. (Xinhua/Tang Yi)

Jitihada za kurejesha mifumo muhimu ya ikolojia pia zimezaa matunda. China imerejesha zaidi ya mu milioni 2.4 (takriban hekta 160,000) za migodi iliyotelekezwa, imerekebisha kilomita 820 za ukanda wa pwani, na kurejesha mu 760,000 (takriban hekta 50,667) za ardhi oevu ya pwani katika kipindi hicho na kwa jumla mu milioni 105 (takriban hekta milioni 7) za ardhi iliyoathiriwa na jangwa zimekarabatiwa, ikiimarisha uwezo wake wa kupambana na hali ya kuenea kwa jangwa na uharibifu wa ardhi.

Picha hii iliyopigwa Julai 11, 2025 ikionyesha mandhari ya mbuga ya taifa ya ardhi oevu ya Mianduhe mjini Hulun Buir, Mkoa Unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China. (Xinhua/Ma Jinrui)

Picha hii iliyopigwa Julai 11, 2025 ikionyesha mandhari ya mbuga ya taifa ya ardhi oevu ya Mianduhe mjini Hulun Buir, Mkoa Unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China. (Xinhua/Ma Jinrui)

Picha hii iliyopigwa Desemba 20, 2025 ikionyesha bata maji kwenye ardhi oevu mjini Sanmenxia, Mkoa wa Henan, katikati mwa China. (Picha na Zhao Yongtao/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Desemba 20, 2025 ikionyesha bata maji kwenye ardhi oevu mjini Sanmenxia, Mkoa wa Henan, katikati mwa China. (Picha na Zhao Yongtao/Xinhua)

Miji ya China imepata maendeleo thabiti katika ubora wa hewa. Mwaka 2024, wastani wa kiwango cha PM2.5 katika miji mbalimbali, kiashiria muhimu cha uchafuzi wa hewa, ulipungua hadi mikrogramu 29.3 kwa kila mita ya ujazo, ikiwa ni punguzo la asilimia 16.3 ikilinganishwa na mwaka 2020. Na uwiano wa siku zenye ubora mzuri wa hewa uliongezeka kwa asilimia 2.4 hadi asilimia 87.2, ikionyesha juhudi zinazoendelea za kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuhimiza uzalishaji na mitindo safi ya maisha.

Picha iliyopigwa Oktoba 21, 2025 ikionyesha trekta za kuvuna zikivuna mpunga kwenye shamba la mpunga, huku treni ya mwendokasi ikipita kwa nyuma, mjini Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China. (Xinhua/Xu Yu)

China pia imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya nishati ya kijani. Kufikia mwisho wa Juni 2025, uwezo wa nchi hiyo wa nishati mbadala ulikuwa umefikia kilowati bilioni 2.159, ikiimarisha zaidi nafasi yake ya kama kinara wa dunia katika uzalishaji wa umeme mbadala.

Picha iliyopigwa Novemba 13, 2025 ikionyesha mradi wa kuzalisha umeme kwa nishati ya jua katika bahari, mjini Dongying, Mkoani Shandong, mashariki mwa China. (Picha na Zhou Guangxue/Xinhua)

Picha iliyopigwa Novemba 13, 2025 ikionyesha mradi wa kuzalisha umeme kwa nishati ya jua katika bahari, mjini Dongying, Mkoani Shandong, mashariki mwa China. (Picha na Zhou Guangxue/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha