Lugha Nyingine
Timu ya madaktari wa China yachangia vifaa tiba kwenye hospitali ya Sudan Kusini
Timu ya 13 ya Madaktari wa China nchini Sudan Kusini jana Jumatatu ilichangia bidhaa za dawa na vifaa tiba kwenye Hospitali ya Mafunzo ya Juba ambayo ni hospitali kuu ya rufaa nchini Sudan Kusini.
Akizungumza katika hafla ya kutoa msaada huo mjini Juba, Waziri wa Afya wa Sudan Kusini Sarah Cleto Rial amesema timu za madaktari wa China zimekuwa zikitoa msaada mkubwa wa kibinadamu kwa miaka mingi tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 2011.
Aidha amesema kwamba timu hizo za madaktari wa China zimefanya kazi kwa karibu na wenzao wa Sudan Kusini kuokoa maisha na kujenga uwezo wa mfumo wa afya, ikiwa ni pamoja na kuanzisha maabara za kisasa na uboreshaji wa vituo vya afya.
Kwa upande wake Balozi wa China nchini Sudan Kusini Ma Qiang amesema kuwa afya ni kiashiria muhimu cha taifa lenye mafanikio na nchi imara, akiongeza kuwa serikali ya China imekuwa ikichukulia ushirikiano wa kimatibabu na kiafya kama eneo muhimu la ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Sudan Kusini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



