Mradi unaojengwa na Kampuni ya China wa kuboresha barabara inayounganisha miji ya Bissau na Dakar waanza

(CRI Online) Desemba 23, 2025

Hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa kuboresha sehemu ya Shoroba za Barabara ya Kuunganisha Bissau na Dakar, inayojengwa na Kampuni ya Uhandisi wa Bandari ya China (CHEC), imefanyika jana Jumatatu huko Tanaff, kusini mwa Senegal.

Awamu ya kwanza ya shoroba za barabara hiyo ina urefu wa jumla wa kilomita 26.4, ikianzia Tanaff na kuendelea hadi kwenye mpaka na Guinea-Bissau. Mradi huo unajumuisha ukarabati wa barabara, uboreshaji wa mifumo ya mifereji ya maji, na kufunga vifaa vya usalama barabarani.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye amesema barabara hiyo itakayoboreshwa itarahisisha usafiri kwa kiasi kikubwa kwa raia wa Senegal na kuongeza safari ya kuvuka mpaka kati ya Senegal na Guinea-Bissau.

Naye naibu meneja mkuu wa CHEC tawi la Afrika Magharibi, Sun Haijun, amesema kampuni hiyo itaendeleza ujenzi kulingana na viwango na ratiba zilizokubaliwa ili kuhakikisha utekelezaji wa mradi huo unakuwa wenye ubora wa hali ya juu na kuhudumia vyema maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha