Lugha Nyingine
Polisi nchini Nigeria waanza operesheni ya kutafuta wasafiri 28 waliotekwa nyara katikati mwa nchi hiyo
(CRI Online) Desemba 24, 2025
Polisi nchini Nigeria imesema wamezindua operesheni ya kutafuta na kuokoa wasafiri 28 waliotekwa nyara Jumapili usiku na watu wenye silaha katika Jimbo la Plateau, katikati mwa nchi hiyo.
Msemaji wa Polisi katika jimbo hilo la Plateau, Alabo Alfred amesema jana Jumanne kwenye mawasiliano na Shirika la Habari la China, Xinhua kuwa, vikosi vya usalama, kwa kushirikiana na taasisi nyingine, vimeanza juhudi za pamoja kuokoa waathirika hao wa shambulizi hilo, lililotokea karibu na jamii ya Wazak katika eneo la Wase.
Amesema kuwa, waathirika hao, wakiwemo wanawake na watoto, waliripotiwa kuwa walikuwa wakisafari kwenda kushiriki hafla ya Kiislamu katika jamii ya Sabon Layi wakati gari walilokuwa wakisafiria lilipozuiliwa.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



