Lugha Nyingine
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Libya na maafisa wengine 4 wafariki katika ajali ya ndege karibu na mji mkuu wa Uturuki
(CRI Online) Desemba 24, 2025
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Libya Mohammed al-Haddad na maafisa wengine wanne wamefariki dunia jana Jumanne jioni kufuatia ndege yao kuanguka kusini mwa Ankara, mji mkuu wa Uturuki.
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Ali Yerlikaya, vikosi vya Gendarmerie vya Uturuki vimepata mabaki ya ndege hiyo, aina ya Falcon 50, karibu na Kijiji cha Kesikkavak katika Wilaya ya Haymana.
Waziri Mkuu wa Libya Abdul-Hamid Dbeibah amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



