Tiexi yajiendeleza kuelekea ustawi mpya kuanzia sauti kubwa ya viwanda vya chuma hadi midundo ya muziki

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 24, 2025

Eneo la Tiexi katika Mji wa Shenyang, Mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China ambalo hapo awali lilijulikana kwa jina la "Ruhr ya Mashariki," lilikuwa moyo wa maendeleo ya viwanda ya kitaifa ya nchi hiyo. Viwanda vyake viliunda mashine ya kwanza ya kerezo, kipande cha kwanza cha chuma cha pua cha China, nembo ya taifa ya kwanza ya madini, na alama nyingine nyingi za maendeleo. Sauti ya mashine hapo awali ilijaa hewani; Hivi leo, midundo inayosikika ni nguvu ya uvumbuzi, matarajio makubwa, na uhai wa maisha.

Katika Jumba la Makumbusho la Viwanda la China, wakati kama unasimama tuli katikati ya injini, mabomba, na kumbukumbu za fahari za wafanyakazi wa vizazi vilivyopita. Mfanyakazi mstaafu Zhang Neng anakumbuka siku zilizokuwa za kung'ara: wafanyakazi wenzake wengi wakielekea kwenye mlango wa kiwanda, wakishika mikononi viboksi vya chakula cha mchana vilivyojaa nyama ya nguruwe na wali, na hisia ya kubeba majukumu ya mji mzima. Simulizi hizo bado zinakuwepo, lakini si kama mabaki ya vitu, bali zimekuwa jiwe la msingi la zama mpya.

Mwaka 2002, Wakati Mji wa Shenyang ulipozindua agizo la maendeleo, majengo mapya marefu yalianza kusimama mjini badala ya viwanda vya zamani vyenye dohari refu. Kampuni kama Shengu Group ziliibuka kutoka kwenye urithi wa viwanda vizito na kubadilika kuwa wavumbuzi wa hali ya juu, ambao kompresa na vipulizio vyake vimekuwa zana za nguvu ya msukumo kwa miradi kote duniani. Sehemu zilizokuwa za mashine za zamani hapo awali, hivi sasa zimekuwa za teknolojia ya kisasa inayosukuma mbele maendeleo ya Tiexi.

Moyo uleule wa uhuishaji mpya unaonekana popote katika Eneo Maalum la Ubunifu wa Utamaduni la Hongmei, ambapo makutano ya mambo ya zamani na ya sasa yanaonekana chini ya kuta za matofali mekundu. Eneo hilo hapo awali lilikuwa Kiwanda cha MSG cha Hongmei; hivi leo, limekuwa ni uwanja wa sanaa, usanifu, na maonesho ya muziki.

"Hatukubadilisha jina," anasema Li Pengfei, mmiliki wa Ghala la Malighafi la Livehouse, ambalo ni mbadala wa sehemu ya kile ambacho kilikuwa nafasi ya ghala la kiwanda. "Vijana wanapokuja hapa kutazama maonesho, nataka wakumbuke mahali hapa palikuwaje hapo awali."

Kutoka mashine zilizounguruma hadi bustani zinazojaa vicheko, Tiexi imepata hali ya kupatana kati ya mambo yake ya zamani na ya siku za baadaye. Wakati watu wake wanapojitokeza —wahandisi, wasanii, wanamichezo, waota ndoto — eneo hilo lililojulikana kwa chuma cha pua, hivi leo linatoa kipaumbele zaidi kwa watu wake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha