Uchumi wa Zimbabwe wakua kwa asilimia 9.64 katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2025

(CRI Online) Desemba 25, 2025

Idara ya Takwimu ya Zimbabwe (ZIMSTAT) jumatano ilisema uchumi wa Zimbabwe umekua kwa asilimia 9.64 katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2025, ikilinganishwa na asilimia 2.28 ya mwaka jana wakati kama huu.

Kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika mjini Harare, meneja wa akaunti za kitaifa wa ZIMSTAT Grown Chirongwe alisema hali hiyo chanya inaonyesha ufufukaji mkubwa wa uchumi kwenye sekta kuu, ukichochewa na kuboreshwa kwa mazingira ya uzalishaji na kuongezeka kwa shughuli katika sekta za uzalishaji bidhaa na utoaji huduma.

Ameongeza kuwa ukuaji huo ulichochewa na utendaji mzuri wa sekta za uchimbaji wa madini na mawe, utengenezaji, fedha na bima, biashara ya rejareja na jumla, na kilimo.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha