Lugha Nyingine
Mlipuko kwenye msikiti nchini Nigeria wasababisha vifo vya watu zaidi ya 10
(CRI Online) Desemba 25, 2025
Mlipuko uliotokea jana jumatano jioni kwenye msikiti mmoja huko Maiduguri, nchini Nigeria umesababisha vifo vya watu zaidi ya 10 na wengine wengi kujeruhiwa.
Waumini walikuwa kwenye sala ya magharibi wakati bomu lililotengenezwa kienyeji (IED) lilipolipuka msikitini katika Soko Kuu la Gamboru. Moshi mzito ulitanda kwenye eneo hilo baada ya mlipuko huo.
Hadi sasa si polisi wala jeshi waliotoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo.
(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



