“Supamaketi ya Dunia” Yiwu yaongeza shamrashamra za sikukuu kote duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 25, 2025

Mfanyabiashara kutoka Kuwait akichagua  sampuli za bidhaa za Krismasi kwenye kituo cha maduka ya biashara ya kimataifa cha Yiwu, Mkoa wa Zhejiang, China tarehe 17, Desemba. (Xinhua/Liu Mingxiang)

Mfanyabiashara kutoka Kuwait akichagua sampuli za bidhaa za Krismasi kwenye kituo cha maduka ya biashara ya kimataifa cha Yiwu, Mkoa wa Zhejiang, China tarehe 17, Desemba. (Xinhua/Liu Mingxiang)

Wakati watu wanapofurahia sikukuu mwishoni mwa mwaka huu, ndipo Mji wa Yiwu wa China, unaojulikana kuwa "Supamaketi ya Dunia" na sehemu kubwa zaidi ya mkusanyiko na usambazaji wa bidhaa za Krismasi, unapoanza kufanya maandalizi ya utoaji bidhaa kwa ajili ya sikukuu ya Krismasi ya mwaka ujao.

Jiang Jiangping, mwenye duka la zawadi na mavazi ya krismasi la Junhong huko Yiwu, ameweka bidhaa mpya za mwaka 2026 kwenye nafasi inayovutia watu macho zaidi. Mfanyabiashara huyu aliyeuza bidhaa husika kwa karibu miaka 30 anafuatilia kwa busara mwelekeo mpya zaidi wa mabadiliko ya soko.

Kamel Mumen, mfanyabiashara kutoka Kuwait, alichagua kofia za mitindio mitano baada ya kuingia kwenye duka hiyo, akauliza kuhusu saizi na bei, akabadilishana na Jiang namba ya simu ili kuwezesha biashara inayofuata. “Nikiwa Yiwu, karibu mahitaji yote ya ununuzi yanaweza kukidhiwa. Aina za bidhaa ni nyingi, wafanyabiashara wana uchangamfu, na biashara huwa na ufanisi sana" alisema Mumen.

Bidhaa za Krismasi za zaidi ya aina 20,000 kutoka Yiwu zinachukua nafasi karibu asilimia 80 kwenye soko la dunia. Kila mwaka bidhaa hizo zinaleta furaha ya Krismasi kwa watu wa nchi na maeneo zaidi ya 100.

"Siku zote kunatoa bidhaa mpya zinazozidi matarajio ya wateja, hii ni moja kati ya mambo muhimu zaidi ya Yiwu kudumisha mvuto wake." Jiang alisema, mwezi Oktoba mwaka huu, viwanda vilianza kusanifu bidhaa mpya kwa mwaka 2026, na wateja wengi wa tangu zamani walituma oda zao za mahitaji ya bidhaa. Hivi sasa, bidhaa za aina mpya zaidi ya 200 zimeshatolewa, na amepanga kutolewa kwa bidhaa za aina mpya 400 hivi.

Picha iliyopigwa tarehe 17, Desemba ikionesha mapambo ya nywele ya “Hello2026” kwenye kituo cha maduka ya biashara ya kimataifa cha Yiwu, Mkoa wa Zhejiang, China. (Xinhua/Liu Che)

Picha iliyopigwa tarehe 17, Desemba ikionesha mapambo ya nywele ya "Hello2026" kwenye kituo cha maduka ya biashara ya kimataifa cha Yiwu, Mkoa wa Zhejiang, China. (Xinhua/Liu Che)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha