Vyombo vitatu vya China vya kuzamia bahari ya kina kirefu vinavyoendeshwa na binadamu vyakamilisha zaidi ya safari 1700 za kuzama kufikia sasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 25, 2025

Watu wakitazama chombo cha kuzamia bahari ya kina kirefu kinachoendeshwa na binadamu cha Fendouzhe (Mjuhudi), kilicho kwenye meli ya utafiti ya Tansuo-1 wakati wa siku ya mwisho ya kufunguliwa kwa umma ya msafara wa pamoja wa utafiti wa bahari ya kina kirefu kati ya China na New Zealand, mji wa Wellington, New Zealand, Machi 21, 2025. (Xinhua/Long Lei)

Watu wakitazama chombo cha kuzamia bahari ya kina kirefu kinachoendeshwa na binadamu cha Fendouzhe (Mjuhudi), kilicho kwenye meli ya utafiti ya Tansuo-1 wakati wa siku ya mwisho ya kufunguliwa kwa umma ya msafara wa pamoja wa utafiti wa bahari ya kina kirefu kati ya China na New Zealand, mji wa Wellington, New Zealand, Machi 21, 2025. (Xinhua/Long Lei)

HAIKOU, Dec. 24 -- Vyombo vitatu vya China vya kuzamia bahari ya kina kirefu vinavyoendeshwa na binadamu vimekamilisha jumla ya safari 1,746 za kuzama kufikia sasa, Taasisi ya Sayansi na Uhandisi wa Bahari ya Kina Kirefu chini ya Akademia ya Sayansi ya China (CAS) ilisema Jumatano.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na taasisi hiyo katika mkutano uliofanyika mjini Sanya, Mkoani Hainan, kusini mwa China, vyombo hivyo vitatu — chombo cha Fendouzhe (Mjuhudi), chombo cha Shenhai Yongshi (Shujaa wa bahari ya kina kirefu) na chombo cha Jiaolong, vinatarajiwa kufanya safari 314 za kuzama katika mwaka huu.

Ni jambo la kutia maanani kuwa, chombo cha Fendouzhe kilitekeleza safari ya kwanza ya China ya utafiti wa sayansi wa bahari ya kina kirefu unaoendeshwa na binadamu katika maeneo ya Bahari ya Aktiki yanayofunikwa na barafu nyingi mwaka huu. Mapema mwaka huu, chombo hicho pia kiliunga mkono safari ya utafiti wa sayansi wa pamoja wa kimataifa katika Mfereji wa Puysegur, uliopo karibu na pwani ya kusini-magharibi ya Kisiwa cha Kusini cha New Zealand.

Chombo kingine Shenhai Yongshi kimetekeleza safari 18 za kuzama kwa ajili ya utafiti wa akiolojia ya bahari ya kina kirefu kwenye eneo la kuhifadhi mabaki ya kale chini ya maji, lililopo kwenye mteremko wa bara wa kaskazini-magharibi mwa Bahari ya Kusini ya China. Aidha, chombo hicho kimefanya kazi kwa kushirikiana na vyombo visivyoendeshwa na binadamu, kusaidia kugunduliwa kwa mabaki mapya ya akiolojia ya bahari ya kina kirefu nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha