Niger yapiga marufuku viza kwa raia wa Marekani

(CRI Online) Desemba 26, 2025

Shirika la Habari la Niger (ANP) limeripoti kuwa Niger imeanza kutekeleza hatua za kulipiza kisasi dhidi ya Marekani wiki hii, ikiweka marufuku kamili ya kutoa viza kwa raia wa Marekani.

ANP imesema kuwa hatua hiyo inafuatia uamuzi wa Marekani wa kuiweka Niger kwenye orodha ya nchi ambazo raia wake hawastahiki tena viza za kuingia Marekani. Niger imesimamisha kabisa na daima kutoa viza kwa raia wote wa Marekani na kuwazuia raia wa Marekani kuingia katika eneo lake kwa muda usiojulikana.

Uamuzi huo uliotolewa katika msingi wa kanuni ya usawa, unaonyesha msimamo wa kidiplomasia unaolenga kulinda uhuru wa kitaifa, na unaashiria mabadiliko katika sera ya kigeni ya Niger.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha